Luke 2

Kuzaliwa Kwa Isa

(Mathayo 1:18-25)

1 aSiku zile Kaisari Augusto alitoa amri kwamba watu wote waandikishwe katika ulimwengu wa Kirumi. 2 b(Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio alikuwa mtawala wa Shamu
Shamu inamaanisha Syria.
).
3Kila mtu alikwenda kuandikishwa katika mji wake alikozaliwa.

4 dHivyo Yusufu akapanda kutoka mji wa Nasiri ulioko Galilaya kwenda Uyahudi, mpaka Bethlehemu, mji wa Daudi, kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo na wa nyumba ya Daudi. 5 eAlikwenda huko kujiandikisha pamoja na Mariamu, ambaye alikuwa amemposa naye alikuwa mjamzito. 6Wakiwa Bethlehemu, wakati wa Mariamu wa kujifungua ukawa umetimia, 7 fnaye akamzaa mwanawe, kifungua mimba. Akamfunika nguo za kitoto na kumlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.

Wachungaji Na Malaika

8Katika eneo lile walikuwako wachungaji waliokuwa wakikaa mashambani, wakilinda makundi yao ya kondoo usiku. 9 gGhafula tazama, malaika wa Bwana akawatokea, nao utukufu wa Bwana ukawang’aria kotekote, wakaingiwa na hofu. 10 hLakini malaika akawaambia: “Msiogope. Kwa maana tazama nawaletea habari njema za furaha itakayokuwa kwa watu wote. 11 iLeo katika mji wa Daudi kwa ajili yenu amezaliwa Mwokozi, ndiye Al-Masihi
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
Bwana.
12 kHii ndiyo itakayokuwa ishara kwenu: Mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa nguo za kitoto na kulazwa katika hori ya kulia ng’ombe.”

13 lGhafula pakawa na jeshi kubwa la mbinguni pamoja na huyo malaika wakimsifu Mungu wakisema,
14 m“Atukuzwe Mungu juu mbinguni,
na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.”

15Hao malaika walipokwisha kuondoka na kwenda zao mbinguni, wale wachungaji wakasemezana wao kwa wao, “Twendeni Bethlehemu tukaone mambo haya ya ajabu yaliyotukia, ambayo Bwana ametuambia habari zake.”

16 nHivyo wakaenda haraka Bethlehemu, wakawakuta Mariamu na Yusufu na yule mtoto mchanga akiwa amelala katika hori la kulia ng’ombe. 17 oWalipomwona yule mtoto, wakawaeleza yale waliyokuwa wameambiwa kuhusu huyo mtoto. 18Nao wote waliosikia habari hizi wakastaajabia yale waliyoambiwa na wale wachungaji wa kondoo. 19 pLakini Mariamu akayaweka mambo haya yote moyoni mwake na kuyatafakari. 20 qWale wachungaji wakarudi, huku wakimtukuza Mungu na kumsifu kwa ajili ya mambo yote waliyokuwa wameambiwa na kuyaona.

21 rHata zilipotimia siku nane, ulikuwa ndio wakati wa kumtahiri mtoto, akaitwa Isa, jina alilokuwa amepewa na malaika kabla hajatungwa mimba.

Isa Apelekwa Hekaluni

22 sUlipotimia wakati wa utakaso wake Mariamu kwa mujibu wa Torati ya Musa, basi Yusufu na Mariamu walimpeleka mtoto Yerusalemu, ili kumweka wakfu kwa Bwana 23 t(kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Bwana, kwamba, “Kila mtoto wa kiume kifungua mimba atawekwa wakfu kwa Bwana”), 24 una pia kutoa dhabihu kulingana na yale yaliyonenwa katika Sheria ya Bwana: “Hua wawili au makinda mawili ya njiwa.”

25 vBasi alikuwako huko Yerusalemu mtu mmoja jina lake Simeoni, ambaye alikuwa mwenye haki na mcha Mungu, akitarajia faraja ya Israeli, na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26 wRoho Mtakatifu alikuwa amemfunulia kuwa hatakufa kabla hajamwona Al-Masihi wa Bwana. 27 xSimeoni, akiwa ameongozwa na Roho Mtakatifu, alikwenda Hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Isa ili kumfanyia kama ilivyokuwa desturi ya Sheria, 28ndipo Simeoni akampokea mtoto mikononi mwake na kumsifu Mungu, akisema:
29 y“Bwana Mwenyezi, kama ulivyoahidi,
sasa wamruhusu mtumishi wako
aende zake kwa amani.
30 zKwa maana macho yangu yameuona wokovu wako,
31ulioweka tayari machoni pa watu wote,

32 aanuru kwa ajili ya ufunuo kwa watu wa Mataifa
na kwa ajili ya utukufu kwa watu wako Israeli.”

33Naye Yusufu na mama yake mtoto wakastaajabu kwa yale yaliyokuwa yamesemwa kumhusu huyo mtoto. 34 abKisha Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, “Mtoto huyu amewekwa kwa makusudi ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ambayo watu watanena dhidi yake, 35 acili mawazo ya mioyo mingi yadhihirike. Nao upanga utauchoma moyo wako.”

36 adTena alikuwako Hekaluni nabii mmoja mwanamke, jina lake Ana binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa mzee sana; naye alikuwa ameolewa na kuishi na mume kwa miaka saba tu, kisha mumewe akafa. 37 aeHivyo alikuwa mjane na umri wake ulikuwa miaka themanini na minne. Yeye hakuondoka humo Hekaluni usiku wala mchana, bali alikuwa akimwabudu Mungu, akifunga na kuomba. 38 afWakati huo huo, Ana alikuja akaanza kusifu, akimshukuru Mungu na kusema habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wakitarajia ukombozi wa Yerusalemu.

39 agYusufu na Mariamu walipokuwa wamekamilisha mambo yote yaliyotakiwa na Sheria ya Bwana, walirudi mjini kwao Nasiri huko Galilaya. 40 ahNaye yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu, akiwa amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.

Kijana Isa Hekaluni

41 aiKila mwaka Yusufu na Mariamu mama yake Isa walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka. 42Isa alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, walipanda kwenda kwenye Sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 ajBaada ya Sikukuu kumalizika, wakati Yusufu na Mariamu mama yake walipokuwa wakirudi nyumbani, Isa alibaki Yerusalemu lakini hawakutambua. 44Wao wakidhani kuwa yuko miongoni mwa wasafiri, walienda mwendo wa kutwa nzima. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa zao na marafiki. 45Walipomkosa walirudi Yerusalemu ili kumtafuta. 46Baada ya siku tatu wakamkuta ndani ya Hekalu, akiwa ameketi katikati ya walimu wa sheria, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 akWote waliomsikia walistaajabishwa na uwezo wake mkubwa wa kuelewa, na majibu aliyoyatoa. 48 alYusufu na Mariamu mama yake walipomwona walishangaa. Mama yake akamuuliza, “Mwanangu, mbona umetufanyia hivi? Tazama, mimi na baba yako tumekuwa tukikutafuta kwa wasiwasi mkubwa kila mahali.”

49 amIsa akawaambia, “Kwa nini kunitafuta? Hamkujua kwamba imenipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?”

50 anLakini wao hawakuelewa maana ya lile alilowaambia.

51 aoNdipo akashuka pamoja nao hadi Nasiri, naye alikuwa mtiifu kwao. Lakini mama yake akayaweka moyoni mwake mambo haya yote. 52 apNaye Isa akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.
Copyright information for SwhKC